Sunday, December 20, 2009

Waridi.

Ua ninakutafuta, tayari ushachanua,
Marashi nanayapata,manukato yavutia,
Ni lini nitakupata,uzuri najivunia,
Waridi nakutafuta, nataka kujichumia.


Niite unionapo, wala usibabaike,
Sijui wapi ulipo,paza sauti iskike,
Ipi ni njia mkato, haraka mimi nifike,
Waridi nakutafuta, nataka kujichumia.


Ni mengi ninayaona, maua ya kupendeza,
Ni lipi lililonona,si kazi ya kubeza,
Waridi ndo lanikuna,ua litaniliwaza,
Waridi nakutafuta, nataka kujichumia.

Waridi ninakusaka,wa maisha jitokeze,
Mbali pia nitafika,ulipo wewe nijuze,
ua umeshapevuka,nakuchuma nikutunze,
Waridi nakutafuta, nataka kujichumia.

Bustanini ninapita,tayari kujichumia,
Tabia itanivuta,ua kufuatilia,
Najua nitalipata,maisha tafurahia.
Waridi nakutafuta, nataka kujichumia.

2 Comments:

Blogger Yasinta Ngonyani said...

Sijui mlipatana maana natoka kwa kaka Fadhy naye kaandika kitu kama hiki. Nadhani si muda mrefu ua hilo litakuwa mikononi mwako. Upendo Daima!!

December 21, 2009 at 3:57 AM  
Blogger Albert Kissima said...

Hahahaha! Nashukuru dada Yasinta kwa baraka zako.

December 22, 2009 at 11:40 PM  

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home