tag:blogger.com,1999:blog-78167877361334705942024-03-05T05:51:53.927-08:00Mwanamalenga.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.comBlogger14125tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-54009723061186926342012-02-14T17:40:00.000-08:002012-02-14T17:56:00.989-08:00NyotaWaridi nakutafuta, shairi niliandika,
Siku nazo zikapita, mwandani nilimsaka,
Sasa nimeshampata, wakati umeshafika,
Nyota wangu unang'aa, daima nitakupenda.

Nyota unanisikia, ninakupenda kwa dhati,
Thamaniyo naijua, ya dhahabu haikuti,
Kuwa nawe najivunia, daima wala sijuti,
Nyota wangu unang'aa, daima nitakupenda.

Ukitaka nitafune, ukitaka unimeze,
Utamuwo wa senene, Wahaya na waeleze,
Si mwembamba si mnene, wa wastani nikujuze,
Nyota wangu unang'aa, daima nitakupenda.

Asante kwa kunijali, thamani kubwa wanipa,
Hujanipenda kwa mali, mapungufu hujakwepa,
Tupitazo zote hali, hutanitenga 'meapa,
Nyota wangu unang'aa, daima nitakupenda.

Washibisha nafsi yangu, Nyota nakuambia,
Waujaza moyo wangu, kwa penzi 'lilotimia,
Heko malaika wangu, kwa penzi li'lotulia,
Nyota wangu unang'aa, daima nitakupenda.

Nyota ninamaanisha, Stella maana yake,
Urembo usiokwisha, hii sifa yake,
Nakupenda wa maisha, ujumbe hima ufike,
Nyota wangu unang'aa, daima nitakupenda.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com2tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-33942715942091618062011-12-23T06:38:00.001-08:002011-12-23T06:56:24.405-08:00Laiti angekuwepoKauli i'lozagaa, ya tamaa kuikata,
U wapi u'lotufaa, twatamani kukufwata,
Nchi inachechemea, ni mengi yanatukuta,
Laiti angekuwepo, mbona Kingunge tunaye?

Ngombale bado tunaye, hima tumtumieni,
Nyerere hatupo naye, fikra'ze zipo vichwani,
Busara'ze ajuaye, Kingunge hoja mezani.
Laiti angekuwepo, Mama Nyerere tunaye.

Mama yetu wa Taifa, ana mengi kutufunza,
Laiti hii ni kashfa, mama bado anaweza,
Kujuta wala si sifa, busara'ze si kubeza,
Laiti angekuwepo, Malecela mbona yupo?

Tokea enzi za baba, alikuwapo Msuya,
Busara alizishiba, wala takrima hakula,
Mbinu bado kazibeba, atumiwe bila hila,
Laiti angekuwepo, mbona wengi bado wapo?

Hebu tuwape nafasi, historia wapakue,
Makovu yake nanasi, utamu'we palepale,
Tuache mawazo hasi, wazee wasaidie,
Laiti angekuwepo, wapo tuwatumieni.

Laiti si neno zuri, twende mbele Tanzania,
Uzalendo ndio siri, tujibidishe kwa nia,
Bila Nyerere si shwari, msemo wa mazoea,
Laiti angekuwepo, mawazoye twatumia?

Wapo wengi wa zamani, enzi zile za Mwalimu,
Ni wachache shairini, wote kuwepo ni ngumu,
Tupeni dira jamani, wa mwalimu mu muhimu,
Laiti angekuwepo, Mpo wengi m'lo tunu.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com2tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-85802123430882927652011-05-20T04:25:00.000-07:002011-05-22T00:48:52.573-07:00Ajali zaepukika!Jamani nisikizeni, nisomeni waungwana,
Nafichani moyoni, lipi lisojulikana,
Ajali tele pomoni, usiku hata mchana,
Madereva mwahusika, ajali zaepukika.

Wa mabasi wamiliki, amueni mtaweza,
Andaeni mikakati, ajali kutokomeza,
Magari muyahakiki, kabla safari kuanza.
Madereva yao haki, wapeni bila kupinda.

Ulevi na muuache, madereva mwahusika.
Subiri hima kukuche, usiku hamtafika.
Sheria mzitumie, mnazitambua fika.
Madereva mtulie, ajali zaepukika.

Ajali zimekithiri, za mabasi si kificho,
Vita si ya hiari, fungueni yenu macho,
Maisha ya wasafiri, bora ya mboni ya jicho,
Kukumbushwa msisubiri, ajali zaepukika.

Abiria kataeni, mwendo uliomkali,
Roho zenu teteeni, si budi kuwa wakali,
Mikanda katika siti, fungeni kwa kila hali.
Wasafiri unganeni, uhai wenu chungeni.

Polisi barabarani, mwahusika siwafichi,
Rushwa sasa acheni, wateteeni wananchi,
Magari ya'lo walakini, hakikisha huyaachi.
Usalama dumisheni, ajali 'taepukika.

Wasanii Five Star, walipoteza maisha,
Ajali twakumbukia, uzembe lisababisha,
Mv bukoba nakumbushia, uzembe umetutosha,
Meli ilielemea, ukweli sitopindisha.

Amani umetutoka, Kessy tulikuhitaji,
Tunalia tunachoka, ajali "mekuwa jaji,
Ajalini 'mekufika, mauti yasotaraji,
Ajali 'metunyang'anya, rafiki yetu mkubwa.

Abiria ushikeni, huu wangu ushauri,
Kulala na epukeni, pindi mnapo safiri,
Magazetini kunani, iwe mwisho wa safari.
Hakuna jipya fanani, yote nayakariri.

Sina tena la ziada, zinaepukika ajali,
Hebu hii iwe mada, namna ya kukabili,
Uhai vema kulinda, tena kwa hali na mali.
Janga si la kawaida, tujipange kukabili.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com7tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-2985942987439245712010-10-04T07:21:00.005-07:002010-10-04T07:21:23.710-07:00Joka mbona huzeeki?Upo toka Tanganyika, hadi sasa Tanzania,
Msingi aliuweka, baba kesha tangulia,
Tayari tungeshafika, Nyerere angendelea,
Joka mbona huzeeki, binafsi nimekuchoka.

Chumvi yote ulokula, tumia basi busara,
Ifike tena pahala, hima iamue kura,
Watu ndio wenye hila, chombo hakina papara,
Joka mbona huzeeki, binafsi nimekuchoka.

Wajengao hicho chombo, kizalendo watafteni,
Ndani kimejaa shombo, chaoshwa kwenye kampeni,
Waambulia kikumbo, watetezi wa maskini,
Joka mbona huzeeki, binafsi nimekuchoka.

Kalamu ninaiacha,wino kamwe hutokwisha,
Joka ondoa makucha, malengo kufanikisha,
Tazama panavyokucha, huna budi kutupisha,
Joka mbona huzeeki, binafsi nimekuchoka.

Uzee busara bwana, zeeka inakubidi,
Kwanini unang'ang'ana , twajua ushafaidi,
Wapeni nao vijana, tuifikie ahadi,
Joka mbona huzeeki, binafsi nimekuchoka.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com1tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-2302246308084589232010-03-29T10:34:00.001-07:002010-03-29T10:41:31.245-07:00Nakutafuta amani.Ajali kila uchao,maisha yanapotea,
wapo wengi hatunao,kwa mola wametangulia,
viongozi soni kwao,lawama twawatupia,
Nakutafuta amani,waongewa sikuoni.

Rushwa iliyokithiri,masikini waonewa,
wakubwa wanakiburi,uchumi wahujumiwa,
pesa kitu jeuri,sheria yapinduliwa,
Nakutafuta amani,waongewa sikuoni.

Ufisadi wabobea,wahusika wanafichwa,
serikali inawajua,majina wanatunziwa,
chamani waogelea,uswahiba twaelewa,
Nakutafuta amani,waongewa sikuoni.

Maji ni kubwa tatizo,watu wanahangaika,
umbali sio mchezo,kina mama wanachoka,
umeme bado gumzo,ni lini taimarika,
Nakutafuta amani,waongewa sikuoni.

Elimu iliyo duni,watoto wataabika,
wanakaa mavumbini,kwa shida wanaandika,
viongozi amkeni,kuonewa tumechoka,
Nakutafuta amani,waongewa sikuoni.

Maisha yaliyo bora,maneno yatamkika,
walitaka hizo kura,kapuni wakatuweka,
twaishi kama chokora,na siku zinakatika,
Nakutafuta amani,waongewa sikuoni.

Hii Tanzania yangu,yenye wingi wa maneno,
amani hili ni jungu,lakwaza si mfano,
amani wapi wandugu,latumika ka'ndoano,
Nakutafuta amani,waongewa sikuoni.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com2tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-19838341130275775692009-12-20T05:44:00.000-08:002009-12-20T05:51:49.374-08:00Waridi.Ua ninakutafuta, tayari ushachanua,
Marashi nanayapata,manukato yavutia,
Ni lini nitakupata,uzuri najivunia,
Waridi nakutafuta, nataka kujichumia.

Niite unionapo, wala usibabaike,
Sijui wapi ulipo,paza sauti iskike,
Ipi ni njia mkato, haraka mimi nifike,
Waridi nakutafuta, nataka kujichumia.

Ni mengi ninayaona, maua ya kupendeza,
Ni lipi lililonona,si kazi ya kubeza,
Waridi ndo lanikuna,ua litaniliwaza,
Waridi nakutafuta, nataka kujichumia.

Waridi ninakusaka,wa maisha jitokeze,
Mbali pia nitafika,ulipo wewe nijuze,
ua umeshapevuka,nakuchuma nikutunze,
Waridi nakutafuta, nataka kujichumia.

Bustanini ninapita,tayari kujichumia,
Tabia itanivuta,ua kufuatilia,
Najua nitalipata,maisha tafurahia.
Waridi nakutafuta, nataka kujichumia.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com2tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-24631185928637594152009-10-09T06:40:00.001-07:002009-10-09T06:40:43.418-07:00MaishaMaisha kweli ni fumbo,lilogumu kufumbua,
Leo lakupiga kumbo,kesho wachekelea,
Punde yezaenda kombo,sharti kujikwamua,
Maisha ndivyo yalivyo,ya kesho huwezi jua.

Maisha yamesheheni,uzuri pia ubaya,
Ungalipo duniani,usiyaonee haya,
Popote yatafuteni,msichoke kusakanya,
Maisha ndivyo yalivyo,ya kesho huwezi jua.

Usitukane wakunga,na uzazi bado upo,
Mlango utafunga,ungali ndani haupo,
Meli maisha tasonga,taachwa hapo ulipo.
Maisha ndivyo yalivyo,ya kesho huwezi jua.

Njiani utayakuta,majabali vizingiti,
Huna budi kuyapita,viunzi havikwepeki,
Kamwe hakuna kujuta,maisha nasbu bahati,
Maisha ndivyo yalivyo,ya kesho huwezi jua.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com2tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-40552289364417349022009-09-21T11:18:00.001-07:002009-09-21T11:18:30.347-07:00MajutoMtegoni nimekwama,pa kutokea sioni,
Pande zote natazama,mkombozi simuoni,
Ndugu zangu wanisema,msaada siuoni,
Siku zangu nazipima,walimwengu kwaherini.

Nahara na kutapika,mwili wote ni vidonda,
Nywele nazo zanyonyoka,natisha nilivyokonda,
Mwili wote unanuka,mauti siwezi shinda,
Saa yangu imefika,najuta niliyotenda.

Ni wengi watafuata,nakiri nilisambaza,
Wengine wameshapita,wengine wazidi cheza,
Wasomi niliwachota,fukara sikubakiza,
Kweli leo ninajuta,nsamehe Mola muweza.

Jamaa wamenitenga,ndugu waninyanyapaa,
Mawazo yananisonga,kutengwa kunaniua,
Lini kusema ntafunga,wote siku wangojea,
Maji yashazidi unga,mauti yanyemelea.

Kwa macho hutamuona,unene sio kigezo,
Vijana mliopona,hima acheni mchezo,
Gonjwa lipo kila kona,acheni vitu vya dezo,
Nakufa bado kijana,kwa Mungu mimi chukizo.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com4tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-16601073894463730772009-09-11T03:32:00.001-07:002009-09-11T03:37:43.137-07:00Jua ni la utosini.Asubuhi kunakucha,na njia ninaishika,
Ninapokwenda naficha,'tasema ntakapofika,
Nitapata ya mchicha?,swali liso na hakika,
Jua ni la utosini,linachoma si utani.

Ni wangu tena ujio,fungua pesa upate,
Chanuo na mafagio,ina njoo nikupake,
Anjifu na mitandio,mikufu pia na pete,
Jua ni la utosini,linachoma si utani.

Huruma siku yapita, ndururu sijainusa,
Watoto mimi najuta,viumbe waso na kosa,
Mitaa ninaipita,wateja spati kabisa,
Jua linanifuata,katu halitaki susa,
Jua ni la utosini,linachoma si utani.

Machinga ndo kazi yangu,mtaa hadi mtaa,
Kazi yanipa machungu,ila sikati tamaa,
Nachoka haki ya Mungu,umande nilikimbia.
Jua ni la utosini,linachoma si utani.

Mlo bahati someni, mwenzenu nilichezea,
Chenga nyingi shuleni,vitabu sikushangaa,
wasomi mataikuni,tuso skuli twaduwaa.
Jua ni la utosini,linachoma si utani.

Siombee umachinga,miguu yote yauma,
Bora jela kutinga,jua la utosi noma,
Pesa haujaichanga,fasta jua lishazama.
Jua ni la utosini,linachoma si utani.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com4tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-36669128268638309802009-09-05T22:00:00.001-07:002009-09-05T22:00:17.965-07:00Wosia wa BabuWajukuu sikizeni,muda wangu umekwisha.
Leo nimewaiteni, muhimu kuwasilisha.
Sikiliza kwa makini,wala sitaki wachosha.

Mkamateni elimu,msimwache aendeze.
Hii ni nguzo muhimu,ili maisha uweze.
Hili ni langu jukumu,nawasihi muutunze.

Cha mwenzako si cha kwako,hilo sharti mlijue.
Tumia akili yako,muulize kapataje.
Kuiba na iwe mwiko,kwa jasho jitafutie.

Kweli kuweni makini,gonjwa lipo mtaani.
vya dezo kataeni,misaada tambueni.
'Siishi kwa tumaini,hasara tele nyumbani.

Maisha si lelemama,juhudi inawapasa.
Msikubali kukwama,sekunde hata lisaa.
Pande zote na tazama,pa kuanza hutokosa.

Kueni wavumilivu,matatizo yakabili.
Katu msiwe wavivu,msibaki na kandili.
Msile ulo mkavu,tulia penye kivuli.

Nguvu zinaniishia,nilosema yashikeni,
Huu ndo wangu wosia,ushikeni akilini.
Dunia itawambia,pembueni kwa makini.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com3tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-45266043502369533582009-07-31T07:37:00.001-07:002009-07-31T07:37:43.860-07:00Dini zetu ni kikwazo.Mola nakupa heshima,ulimwengu uliumba.
leo mimi natazama,wapo waloshayafumba.
Kisa wazi nakisema,mimi na wangu mchumba.
dini zetu ni kikwazo,e Mola tusaidie.

Sio siri nampenda,shairi nimeandika.
kwa mwingine sitoenda,mistari niliishuka.
vishawishi nitashinda,nilisema na hakika.
dini zetu ni kikwazo, e mola tusaidie.

Mapenzi hayana dini,kabila wala hayana.
semi hizi kulikoni,hatarini kuachana.
ya kweli yangu imani,kamwe siwezi ikana.
Mwenzangu yake imani,msimamo kesha weka.
dini zetu ni kikwazo, e Mola tusaidie.

Wazaziwe wamfunza,kiburi wamjazia.
dini yake kuitunza,msimamo wamwekea.
wazaziwe wanibeza,kifupi wanichukia.
dini zetu ni kikwazo, e Mola tusaidie.

Baba mama walionya,kupenda kuliniteka.
Tayari walishaona,uzoefu 'litumika.
yakwao sikuyaona,kupenda kulifunika.
Dini zetu ni kikwazo, e Mola tusaidie.

Mwanangu hebu tulia,wa diniyo tampata.
chunga kutokujutia,matatizo tayapata.
haya nayakumbukia,rafiki alinisuta.
dini zetu ni kikwazo, e Mola tusaidie.

Njia panda bado nipo,sina pa kuelekea.
Nipeni njia mkato,mapenzi nayajutia.
Hima popote ulipo,ushauriwo "tapokea.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com3tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-91206737114725192462009-07-24T03:53:00.000-07:002009-07-24T04:00:04.028-07:00Sio siri nakupenda.Miaka ilishapita,magumu niliyavuka.
Visiki nilivipita,wa maisha kumsaka.
Nilijua 'tampata,papara sikuzitaka.
Sio siri nakupenda,kwa mwingine sitoenda.

Natamani uwe wangu,niambie nitulie.
Ilikuwa siri yangu,imebidi nikujuze.
Niwambie ndugu zangu,baraka watujalie.
Sio siri nakupenda, kwa mwingine sitoenda.

Usiku hata mchana,nakuwaza nisikie.
Mapenzi yalomapana,nipokee unifiche.
Sio leo wala jana,penzi langu litambue.
Sio siri nakupenda,kwa mwingine sitoenda.

Sina sababu kupenda, ulivyo waniridhisha.
Sitake mimi kukonda,wewe ndo yangu maisha.
Naapa sitokutenda,hima sitobabaisha.
sio siri nakupenda, kwa mwingine sitoenda.

Tamati nimeifika,nambie unachowaza.
Kwako nimefika,sijui kama wakwanza.
Wewe utachotamka,moyoni tanituliza.
Sio siri nakupenda, kwa mwingine sitoenda.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com2tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-4759752552138512422009-07-16T22:19:00.000-07:002009-07-16T22:28:46.746-07:00YATIMA JAMA HURUMA.Yatima waso hatia,huruma napowakuta.
mlo wajitafutia,si hakika kuupata.
jalalani kuchokona,chochote watachopata.
yatima jama huruma,sio lao kusudio.

Magonjwa yawaandama,hakuna wa kuwatibu.
nani wa kuwatazama,maradhi yawaadhibu.
na chawa wawaandama,malazi yaso adabu.
yatima jama huruma,sio lao kusudio.

Mikononi mwa polisi,mkong'oto kama kazi.
maisha ya wasiwasi,watumiwa kwenye wizi.
zawakosa na risasi, kifo kipo waziwazi.
yatima jama huruma,sio lao kusudio.

Wengine pia hubakwa,ukimwi rahisi kupata.
Wengine hulawitiwa,makubwa na huwakuta.
miili yao yauzwa,
wengine kunufaika.
Yatima jama huruma, sio lao kusudio.

Wazazi nisikieni,tulieni msiruke,
ukimwi upo jamani,chunga usiwamalize.
malezi ni ya wazazi, walimwengu wako bize.
yatima jama huruma, sio lao kusudio.

Vijana siwasahau,kila jambo na wakati.
katu usijisahau,kuzaa kabla wakati.
wala usijejaribu,ngono siipe nafasi.
yatima jama huruma,sio lao kusudio.

Yapo mengi yawasibu,siwezi yote eleza.
Sote na tunawajibu,kutoa tunachoweza.
Elimu kwao muhimu,hamasika kuwatunza.
Yatima jama huruma, sio lao kusudio.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com3tag:blogger.com,1999:blog-7816787736133470594.post-38267607780238480822009-07-14T00:49:00.000-07:002009-07-14T00:50:32.461-07:00NINI WAMETUFANYIA?Uchaguzi mbili kumi,huo hapo wajongea.
Waja kuisaka kumi, wako waliolowea.
wametufanyia nini, jibu sharti kutupatia.
tuamke wajameni,tuchague wa kutusaidia.
Kura fika haki yako,umpendaye mchague.
hupotezi muda wako,uhakika wa badae.
nini wametufanyia,waulizwe bila woga.

Tarehe itawadia,kampeni kuzipiga.
Waongo utawajua,'tazijua zao soga.
uwezo kuzingatia, zawadi wakizimwaga.
nini wametufanyia,waulizwe bila woga.

Takrima usikubali,mzalendo 'ndo kigezo.
yule atayekujali, hela isiwe kigezo.
Usiukubali wali,wala tisheti za dezo.
nini wametufanyia,waulize bila woga.

Wageni watatujia,yakwao watatwambia.
nini watatufanyia,bayana kutuwekea.
zipi 'takuwa hatua,wasipotutimizia?
nini wametufanyia,waulizwe bila woga.

Kalamu naweka chini,jamani tuwe makini.
somo lipo akilini,mitano hiyo ni mingi.
nne moja fomesheni,kamchezo kasomeni.
nini wamefanya,waulizwe bila woga.Albert Kissimahttp://www.blogger.com/profile/17395730843653433393noreply@blogger.com4