Friday, July 24, 2009

Sio siri nakupenda.

Miaka ilishapita,magumu niliyavuka.
Visiki nilivipita,wa maisha kumsaka.
Nilijua 'tampata,papara sikuzitaka.
Sio siri nakupenda,kwa mwingine sitoenda.


Natamani uwe wangu,niambie nitulie.
Ilikuwa siri yangu,imebidi nikujuze.
Niwambie ndugu zangu,baraka watujalie.
Sio siri nakupenda, kwa mwingine sitoenda.


Usiku hata mchana,nakuwaza nisikie.
Mapenzi yalomapana,nipokee unifiche.
Sio leo wala jana,penzi langu litambue.
Sio siri nakupenda,kwa mwingine sitoenda.


Sina sababu kupenda, ulivyo waniridhisha.
Sitake mimi kukonda,wewe ndo yangu maisha.
Naapa sitokutenda,hima sitobabaisha.
sio siri nakupenda, kwa mwingine sitoenda.


Tamati nimeifika,nambie unachowaza.
Kwako nimefika,sijui kama wakwanza.
Wewe utachotamka,moyoni tanituliza.
Sio siri nakupenda, kwa mwingine sitoenda.

2 Comments:

Blogger Fadhy Mtanga said...

Tamati sitoifika, mapenzi hayana mwisho,
Mapenzi yaongezeka, kila ifikapo kesho,
Kwangu homa inashuka, kwako tabibu spesho,
Nakupenda sitochoka.

July 26, 2009 at 10:18 AM  
Blogger Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kupenda kuna gharama zake. Na kuna watu wanaweza kufanya kila kitu kwa saababu ya kupenda.

July 31, 2009 at 8:45 AM  

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home