Tuesday, July 14, 2009

NINI WAMETUFANYIA?

Uchaguzi mbili kumi,huo hapo wajongea.
Waja kuisaka kumi, wako waliolowea.
wametufanyia nini, jibu sharti kutupatia.
tuamke wajameni,tuchague wa kutusaidia.
Kura fika haki yako,umpendaye mchague.
hupotezi muda wako,uhakika wa badae.
nini wametufanyia,waulizwe bila woga.

Tarehe itawadia,kampeni kuzipiga.
Waongo utawajua,'tazijua zao soga.
uwezo kuzingatia, zawadi wakizimwaga.
nini wametufanyia,waulizwe bila woga.


Takrima usikubali,mzalendo 'ndo kigezo.
yule atayekujali, hela isiwe kigezo.
Usiukubali wali,wala tisheti za dezo.
nini wametufanyia,waulize bila woga.


Wageni watatujia,yakwao watatwambia.
nini watatufanyia,bayana kutuwekea.
zipi 'takuwa hatua,wasipotutimizia?
nini wametufanyia,waulizwe bila woga.

Kalamu naweka chini,jamani tuwe makini.
somo lipo akilini,mitano hiyo ni mingi.
nne moja fomesheni,kamchezo kasomeni.
nini wamefanya,waulizwe bila woga.

4 Comments:

Blogger Fadhy Mtanga said...

Kweli tupu umesema, nami nakukubalia,
Yapaswa sana hekima, katika kufikiria,
Tuzingatie mapema, katika kuyaamua,
Uchaguzi unakuja, tuchague walo bora.

Tumefurahi Kissima, watu kuwakumbushia,
Tuseme tupo wazima, tunapo pa kusemea,
Tuchague walo wema, siyo wa kutuibia,
Uchaguzi unakuja, tuchague walo bora.

July 14, 2009 at 5:48 AM  
Blogger Yasinta Ngonyani said...

Kazi nzuri, ni kweli kama hatutachagua walio bora basi tutabaki kama tulivyo. Ni wakati wa mabadiliko sasa

July 14, 2009 at 7:35 AM  
Blogger Mzee wa Changamoto said...

Swadaktaaaa! Nimewasili na japo mie malenga yangu ni ya "kuvuta kwa manati", lakini ntajitahidi kuweka mbili tatu kila kichwa kinaporuhusu. Hahahahahahaaaaaaaaa.
Pole kwa kupotea kwangu.
Pamoja Daima

July 14, 2009 at 9:27 AM  
Blogger Albert Kissima said...

Kaka Fadhy, dada Yasinta na Kaka Mubelwa, karibuni sana na nawashukuru kwa kukitembelea kibara hiki kipya.

July 14, 2009 at 11:41 AM  

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home