Saturday, September 5, 2009

Wosia wa Babu

Wajukuu sikizeni,muda wangu umekwisha.
Leo nimewaiteni, muhimu kuwasilisha.
Sikiliza kwa makini,wala sitaki wachosha.


Mkamateni elimu,msimwache aendeze.
Hii ni nguzo muhimu,ili maisha uweze.
Hili ni langu jukumu,nawasihi muutunze.

Cha mwenzako si cha kwako,hilo sharti mlijue.
Tumia akili yako,muulize kapataje.
Kuiba na iwe mwiko,kwa jasho jitafutie.


Kweli kuweni makini,gonjwa lipo mtaani.
vya dezo kataeni,misaada tambueni.
'Siishi kwa tumaini,hasara tele nyumbani.

Maisha si lelemama,juhudi inawapasa.
Msikubali kukwama,sekunde hata lisaa.
Pande zote na tazama,pa kuanza hutokosa.

Kueni wavumilivu,matatizo yakabili.
Katu msiwe wavivu,msibaki na kandili.
Msile ulo mkavu,tulia penye kivuli.

Nguvu zinaniishia,nilosema yashikeni,
Huu ndo wangu wosia,ushikeni akilini.
Dunia itawambia,pembueni kwa makini.

3 Comments:

Blogger Fadhy Mtanga said...

Babu tumekusikia, yote uliyoyasema,
Nasi tutazingatia, manenoyo ya hekima,
Twajua watutakia, maisha yalo salama.

Babu usiwe na wasi, wajukuu twajitunza,
Twayaepuka maasi, twajua yatatuponza,
U mfano kwetu sisi, kwako mema twajifunza.

Babu uwe na amani, lakini utuombee,
Tusiwe majaribuni, uovu utukemee,
Uwe sana duniani, mwenyewe ujionee.

Ahsante sana babu.

September 5, 2009 at 11:19 PM  
Blogger Albert Kissima said...

Kaka Fadhi 'mekusoma,ulongea ni hekima,
Babu niliyoyasema,ni machache ukipima,
mjukuu umesema,kwa kina umeeleza.

September 6, 2009 at 9:54 AM  
Blogger Unknown said...

Napenda mizani miye....

May 29, 2021 at 10:30 AM  

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home